St. Teresia wa Avila Pre & Primary School inapenda kuwakaribisha wazazi na walezi wote kuandikisha watoto wao kwa mwaka wa masomo 2025. Shule yetu ni ya kutwa, inayomilikiwa binafsi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, na imejipambanua kwa utoaji wa elimu bora kwa watoto wa jinsia zote kuanzia awali hadi darasa la tano.
Ngazi Zinazopatikana:
-
Awali (Nursery/Pre-Unit)
-
Darasa la 1 hadi la 5
Nafasi za kujiunga zipo wazi kwa watoto wa umri wa kuanzia miaka 3. Tunasajili wanafunzi wapya kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2025. Tunapokea wanafunzi kutoka dini, makabila, na asili mbalimbali.
Sifa za Kipekee za Shule Yetu:
✅ Tunapokea wanafunzi wa DINI ZOTE
✅ Walimu wenye uzoefu na umahiri wa hali ya juu
✅ Ada nafuu na inayolipwa kwa awamu
✅ Mazingira ya kujifunzia yaliyoboreshwa kitaaluma
Sera ya Usajili:
Kabla ya kujiunga, mzazi au mlezi pamoja na mwanafunzi wanapaswa kuhudhuria mahojiano maalum. Watatakiwa kuwasilisha cheti cha kuzaliwa na picha ndogo 3 kwa ajili ya usajili.
Mawasiliano:
📍 Shule iko Kibwegere-Kibamba, Manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam
📞 +255 742 226 356 | +255 788 771 701
📧 st.teresiawaavilaschool@gmail.com
📱 Instagram: @st.teresiawaavilaschool
🌍 Website: www.stteresiawaavilaschool.ac.tz
Jiunge na familia ya St. Teresia wa Avila – mahali ambapo elimu, maadili na imani vinakutana kuunda kizazi chenye maono!

Leave a Reply